Mapishi ya mandi ya kuku

Mandi ya kuku

225

Mahitaji

 • Vikombe 2 mchele – uroweke dakika 10
 • Vipande 2 vya kuku (kila 1 paja na mguu)
 • Kitunguu maji 1
 • Kitunguu saum na tangawizi kjk 1
 • Kidonge cha supu cha kuku 1
 • Matunda makavu kiasi (nimetumia lozi)
 • Bizari nyembamba kjk 1 kikubwa
 • Mbegu za giligilani kjk 1 kidogo
 • Pilipili manga nusu kjk cha chai
  Iliki chembe 4
 • Malasini vipande 2 vya kiasi
 • Bizari ya mchuzi nusu kjk cha chai
 • Chumvi kiasi
 • Mafuta ya kupikia vjk 5
 • Paprika ya unga kjk 1 (si lazima)

MATAYARISHO

1.Kwenye pan kavu, kaanga lozi au zipashe moto kwa dakika 2 mpaka 3, ziweke pembeni

2.Kwenye pan hiyo hiyo, weka spices zote isipokua paprika na bizari ya mchuzi. Zikaange kwa moto mdodo mdogo kwa dakika 2 au mpaka uone zimeanza kutoa harufu yake, wacha zipoe kwa dkk 1. Zosage kwa blender au zitwangwe kwa kinu mpaka ziwe unga

3.Zigawe sehem 2 sawa sawa, sehem 1 tutaitumia moja kwa moja, sehem ya 2 iweke tutaitumia badae

watch full video here;

4.Chukua sehem 1 ya spices uchanganye na kjk 1 cha mafuta au maji ya limau mpaka upate mchanganyiko mzito (paste), pakaza kwenye kuku wote na wacha akolee kwa dakika 15 mpaka 30

5.Kwenye sufuria tia mafuta ya kupikia vijiko 3, kaanga vitunguu maji kwa dakika 2 visipige rangi sana. Tia kuku uwakaange au uwawache wawivie mafuta kwa dakika 2 mpaka kila upande. Baada ya hapo tia maji ya kutosha kuwivisha kuku

6.Kuku akiwiva tu mtoe kwenye sufuria na muweke pembeni

7.Kwenye supu ilobaki kwenye sufuria, tia kitunguu saum na tangawizi, bizari ya mchuzi na kidonge cha supu. Hakikisha supu ya kuku ni kiasi ya kuwivishia mchele vikombe Sasahivi, tia mchele kwenye supu ya kuku na upike kwa moto mdogo mdogo bila kukoroga sana mpaka wali unakauka, weka matunda makavu na ufunike kwenye moto mdogo mdogo sana ZINGATIO: unaweza kuengeza chumvi ikihitajika

8.Wakati huo huo, chukua spices fungu la pili, changanya na mafuta vijiko 2, chumvi pamoja na paprika powder mpaka ichanganyike vizuri ( kumbuka paprika sio lazima, nimetumia kwa kumfanya kuku awe na rangi pamoja na pilipili) unaweza kutumia rangi ya chungwa au manjano pamoja kufanya kuku wako awe na rangi na Pilipili ya unga) Ukishakufanya mchanganyiko wako, pakaza vizuri kwenye kuku wako uliempika Mchome kwa makaa au oven kwa dakika 15 mpaka 20.

9.Akimaliza muweke kwenye sufuria la wali

10.Washa kipande cha mkaa, kikishakiwaka kiweke kwenye kibakuli kidogo na utie kwenye sufuria la mandi na utie kijiko 1 cha mafuta (kwenye mkaa wa moto) na ufunike haraka kuzuwiya moshi usitoke nje ya sufuria. Fukiza kwa dakika 2 mpaka 3 na wali wa wako wa mandi upo tayari

11.Tayari kwa kula na wekea na majani ya giligilani ukipenda

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Leave A Reply

Your email address will not be published.